Hosea 5:6-15

6 aWakati wanapokwenda na makundi yao
ya kondoo na ngʼombe
kumtafuta Bwana,
hawatampata;
yeye amejiondoa kutoka kwao.
7 bWao si waaminifu kwa Bwana;
wamezaa watoto haramu.
Sasa sikukuu zao za Mwandamo wa Mwezi
zitawaangamiza wao
pamoja na mashamba yao.

8 c“Pigeni tarumbeta huko Gibea,
baragumu huko Rama.
Paza kilio cha vita huko Beth-Aveni,
Beth-Aveni maana yake Nyumba ya Ubatili (au Uovu), jina lingine la Betheli kwa dhihaka.

ongoza, ee Benyamini.
9 eEfraimu ataachwa ukiwa
katika siku ya kuadhibiwa.
Miongoni mwa makabila ya Israeli
ninatangaza lile ambalo halina budi kutukia.
10 fViongozi wa Yuda ni kama wale
wanaosogeza mawe ya mpaka.
Nitamwaga ghadhabu yangu juu yao
kama mafuriko ya maji.
11 gEfraimu ameonewa,
amekanyagwa katika hukumu
kwa kuwa amekusudia kufuatia sanamu.
12 hMimi ni kama nondo kwa Efraimu,
na kama uozo kwa watu wa Yuda.

13 i“Wakati Efraimu alipoona ugonjwa wake,
naye Yuda vidonda vyake,
ndipo Efraimu alipogeukia Ashuru,
na kuomba msaada kwa mfalme mkuu.
Lakini hawezi kukuponya,
wala hawezi kukuponya vidonda vyako.
14 jKwa maana nitakuwa kama simba kwa Efraimu,
kama simba mkubwa kwa Yuda.
Nitawararua vipande vipande na kuondoka;
nitawachukua mbali,
na hakuna wa kuwaokoa.
15 kKisha nitarudi mahali pangu
mpaka watakapokubali kosa lao.
Nao watautafuta uso wangu;
katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.”
Copyright information for SwhNEN